Picha Kwa Hisani – Akothee Instagram Page
Mwanamuziki na mfanyabiashara Esther Akoth maarufu kama Akothee anatamba mitandaoni baada ya kuorodheshwa kati ya wasanii 20 tajiri zaidi bara la Afrika na Jarida la Forbes.
Akothee ambaye ni nambari 15 kwenye orodha hiyo, ndio mwanadada wa kwanza Afrika na msanii wa kwanza Afrika ya Mashariki.
Mwanamuzki huyo mwenye umri wa miaka 40, ameshindwa kuficha hisia zake na kuchapisha jumbe za furaha katika ukurasa wake wa Instagram.
Picha Kwa Hisani – Akothee Instagram Page
Utajiri wake unaonekana kwenye majumba yake ya kifahari aliyoyajenga ndani na nje ya nchi.
Akothee ndiye mwanamuziki pekee kutoka Kenya kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Youssou N’Dour kutoka Senegal akiwa na utajiri wa karibu shilingi billioni moja.
Mwanabiashara huyo alipakia picha ya orodha hiyo, huku akisema kuwa msanii Akon ambaye ni nambari mbili, sasa anamtambua.
Picha Kwa Hisani – Akothee Instagram Page
Miongoni mwa wasanii walioorodheshwa ni Wizkid, Davido, Burnaboy, Rudeboy, Mr. P, Bobby Wine, Black Coffee, Timaya na Dbanj.
Hongera kwa Akothee.