Msanii Nyota Ndogo amefichua kuwa Akothee amempa msaada mkubwa katika kutafuta wapangaji wa nyumba zake za kukodi.
Kupitia kwa ujumbe mrefu aliouweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nyota Ndogo amesema kuwa Akothee ndiye aliyemtia moyo azidi kupost kuhusu biashara yake ya kukodi nyumba baada ya watu kumkejeli alipopost nyumba hizo mtandaoni.
“Nilipokua najenga nyumba zangu zakukodisha nikipost insta wengine ooh watuonyesha ooh sijui mambo mengine ficha ni pasonal sana kitu sikuelewa biashara utaficha? Unatarajia umuuzie nani ukishaificha?so kuna watu usoma comment kwa wall na kuamua tu kunyamaza but @akotheekenya alinipigia simu akaniambia wewe mwanamke endelea kusikiza watu na maisha yako hayatasonga post kitu unajiskia kupost post hizo nyumba sana ndio biashara na akachukua hizo video akapost kwakwe kunipa sapoti,” umesema ujumbe huo.
Aidha ameendelea kusema kuwa ipo nyumba yake moja ambapo mpangaji aliingia hivi majuzi aliyekiri kuwa alifahamu kuwepo kwa nyumba hiyo kupitia ukurasa wa Akothee.
” Tulipomaliza kuongea akaniambia nimezitafuta nyumba Zako baada ya kuziona kwa @akotheekenya,” umeendelea kueleza ujumbe huo.
Taarifa na Dominick Mwambui.