Akina mama katika eneo la Matuga kaunti ya Kwale wamehimizwa kutohofia lolote na badala yake kuwapeleka watoto wao hospitali ili kupata chanjo ya maradhi mbalimbali.
Afisa wa Afya katika kituo cha afya cha Chitsanze, Catherine Gacheria amesema chanjo ni kinga ya maradhi mbalimbali kwa watoto.
Kauli yake imejiri baada ya tetesi kuibuka kuwa kuna baadhi ya akina mama ambao wanahofia kuwapeleka watoto wao hospitalini kwa chanjo za maradhi mbalimbali, wakihofia kupata na virisi vya Corona.