Moses Mwenda ndiye mshindi wa mashindano ya E Sports Tournament mkoa wa Pwani yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom katika kaunti ya Mombasa baada ya kumnyuka Fahad Ali mabao 3-1.
Kulingana na mshirikishi katika shirika hilo Peter Kuria amesema wanampango wa kuufanya mchezo huo kuwa wa kitaifa ili kuwapa fursa vijana wenye talanta hiyo kutambulika.
Aidha Kuria ametaja michezo hiyo kuchezwa na vijana wengi kisha mwishowe kukosa namna za kuendeleza talanta zao kwa kukosa jukwaa la kuonyosha talanta hizo.
Moses kutoka mjini Mombasa alijinyakulia 50,000 pesa taslim huku mshindi wa pili Fahad Ali aliyefuzu kutoka Mariakani alinyakua 30,000 huku Maranda Mark akizoa 20,000 katika nafasi ya tatu baada ya kufungwa mabao 3-1 na Fahad Ali.