Story by Mwanaamina Fakii –
Mhudumu mmoja wa bodaboda ameaga dunia huku abiria wengine watatu waliokuwa wameabiri bodaboda hiyo wakinusurika katika ajali ya barabarani iliyohusisha bodaboda hiyo na gari ndogo aina ya Nissan katika eneo la Tiwi kaunti ya Kwale.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Oloo amesema abiria walionusurika wamepata majeruhi madogo na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Msambweni.
Oloo amezidi kuwatahadharisha wahudumu wa boda boda dhidi ya kubeba abiria zaidi ya mmoja na vile vile kutoendesha bodaboda hizo kwa mwendo wa kasi wakati wanapokuwa barabarani.
Hata hivyo amewawonya vijana katika eneo la Tiwi ambao walijaribu kufunga barabara na kuandamana kufuatia ajali hiyo, akisema walitatiza pakubwa shuhuli za usafiri.