Picha kwa Hisani –
Mahakama ya Mombasa imeagiza mbunge wa malindi Aisha Jumwa na mshatakiwa mwenza kwenye kesi ya mauaji inayowakabili Geoffrey Otieno wazuilewe katika kituo cha polisi cha bandari mjini Mombasa hadi siku ya alhamisi juma hili.
Akitoa uamuzi huo Jaji Njoki Mwangi amesema Jumwa atafanyiwa vipimo vya akili siku ya kujamano,kabla ya kurejeshwa tena mahakamani siku ya alhamisi juma hili kujibu mashataka ya mauaji yanayomkabili kulingana na sheria ya nchi.
Jaji njoki vile vile wakati wa kusikilizwa kwa kesi hio hii leo amesema wawili hao wanazuiliwa huku mahakama ikifanya majadiliano kuhusu suala la kuachiliwa kwa dhamana.
Itakumbukwa kwamba mkurugenzi wa mashataka ya umma nchini Noordin Hajj aliidhinisha mashataka ya mauaji kwa mbunge huyo wa Malindi juma lililopita akisema amekusanya ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma dhidi ya mbunge huyo.
Jumwa anakabiliwa na tuhuma za mauaji ya mauaji Ngumbao Jola yaliotekelezwa mwaka 2019 wakati wa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa wadi ya Ganda kaunti ya Kilifi,na kesi hio imeratibiwa kusikizwa tena tarehe 22 mwezi huu wa oktoba.