Viongozi wa kaunti ya Kilifi, sasa wanazitaka idara mbalimbali, viongozi wa kidini, maafisa wa usalama pamoja na mashirika ya kijamii kuhakikisha ongezeko la visa vya mimba za mapema vinadhibitiwa.
Akiongea katika eneo la Takaye kule Malindi kaunti ya Kilifi, Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amesema takwimu zimetolewa hivi majuzi zinazoonyesha kuwa kaunti ya Kilifi ina jumla ya visa elfu 13 vya wanafunzi waliotungwa uja uzito.
Aisha amehoji kuwa ni lazma hatua mwafaka ziidhinishwe ili kukabiliana na hali hiyo na wala sio kuwalaumu viongozi kutokana na dhana kuwa wamesahau majukumu yao.
Mbunge huyo vile vile amewalaumu maafisa wa polisi kutokana na kile alichokitaja kuwa wamezembea kutekeleza majukumu yao na kupeana vibali vya sherehe za usiku maarufu Disco Matanga na kuchangia dhulma za kijinsia.
Taarifa na Charo Banda.