Siku moja baada ya Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa Karisa kutemwa rasmi kutoka kwa chama cha ODM ametishia kuelekea mahakamani kutafuta haki.
Akizungumza eneo la Kakuyuni Jumwa amesisitiza kuwa japo ODM inazo sheria zake sheria ya nchi pia iko na kwamba atafuata utaratibu wa kisheria kupiga vita hivyo ambavyo vimemuandama kwa sasa.
Jumwa amedokeza kuwa hajaridhika na hatua hiyo na kwamba ametilia shaka mno kuhusu ni jinsi gani ODM ilichukua uamuzi wa kumtimua yeye huku wakimpa msamaha Mbunge wa Msambweni Suleiman Dori.
Jumwa amehoji kuwa huenda njia za ufisadi zilitumika kumtimua na kwamba yote ambayo yamemkumba ni sawia na mzaha kwake na kwamba yeye angali imara kisiasa.
Taarifa na Charo Banda.