Story by Mwahoka Mtsumi –
Naibu Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Ali ameapishwa rasmi kuchukua nafasi ya ugavana.
Ahmed ameapishwa na Jaji Said Chitembwe katika makao makuu ya serikali ya kaunti ya Wajir katika kikao kilichohudhuriwa na wakaazi wa kaunti ya Lamu, Wawakilishi wa wadi katika kaunti hiyo na viongozi mbalimbali.
Baada ya kuapitishwa Gavana huyo mpya Ahmed Ali ameahidi kuwaunganisha wakaazi wa kaunti ya Wajir, kushuhulikia swala la afya, kuhakikisha huduma za maendeleo zinawafikia wananchi huku akiwaomba wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana na serikali yake.
Ahmed amechukua hatamu ya uongozi kutoka kwa Abdi aliyebanduliwa Mamlakani baada ya Wawakilishi wa wadi wa kaunti hiyo kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na bunge la seneti siku ya Jumatatu likaidhinisha uamuazi huo.