Shirika la huduma za feri nchini limezindua upya kivuka cha Mtongwe ili kukabiliana na masongamano wa magari na abiria katika kivuko cha feri cha Likoni.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Bakari Hamis Gowa amesema hatua hiyo itasaidia kuzikabili changamoto zinazoshuihudiwa katika kivuko cha Feri cha Likoni kutokana na idadi ya watu inayozidi kuongezeka.
Bakari amesema kuzinduliwa upya kwa kivuko cha Mtongwe kutawezesha kuinua viwango vya biashara mbalimbali sawia na kurahisisha shuhuli za uchukuzi.
Kwa upande wao wananchi wanaotumia kivuko cha Likoni wamesifia kuzinduliwa upya kwa kivuko cha Mtongwe, wakisema kitarahisisha shuhuli za usafiri.
Taarifa na Hussein Mdune.