Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi ya Bidiinimole kaunti ya Kwale amapeta afueni baada kupata ufadhili wa matibabu katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani, baada ya jicho lake moja kufura na kuharibika kabisa.
Samson Mwangale mwanafunzi wa darasa la 7 alilazimika kuwacha masomo baada ya kukabiliwa na matatizo ya ubongo ambayo vile vile yaliathiri jicho lake moja japo sasa amefanyiwa upasuaiji na anaendelea kupata afueni.
Akizungumza na Radio Kaya katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani ambako Mwangale ambaye pia ana ulemavu wa ngozi anaendelea kupata nafuu, Daktari Renson Zoka ambaye ni mtaalam wa tiba ya macho amesema Mwangale anaendelea vyema.
Naye Afisa wa uhusiano mwema wa kampuni ya kutengeneza saruji ya Mombasa Cement ambaye pia ni Mwakilishi Wadi ya Tudor Samiir Baloo akisema watagharamia mahitaji zaidi ya mwanafunzi huyo kwa matibabu yake yamegarimu shilingi laki 4.