Picha kwa Hisani –
Afisi ya mwanasheria mkuu nchini imepokea magari 41 yatakayosambazwa katika kaunti mbali mbali ili kuendeleza huduma zitakazofanikisha utekelezwaji wa sheria na haki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo jijini Nairobi wakili mkuu wa serikali (Solicitor General) Kennedy Ogeto amesema hatua hio itarahisishia wananchi katika kaunti zote kupata huduma kwa urahisi.
Ogeto amesema magari hayo yatasaidia maafisa wa afisi ya mkuu wa sheria nchini kuiwakilisha vyema serikali katika mahakama za humu nchini ikizingatiwa kwamba kwa sasa kuna kesi nyingi zinazowasilishwa mahakamani dhidi ya serikali.
Wakili huyo mkuu wa serikali aidha amesema wanalenga kusambaza huduma za afisi hio katika kaunti zote 47 nchini.