Kumezuka kizazaa katika gereza la Malindi kaunti ya Kilifi baada ya afisaa mmoja mwenye cheo cha Constable kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya na wakubwa wake.
Taarifa kutoka kwa walioshughudia kisa hicho zimefichua kwamba afisa huyo kwa jina Peter Ndirangu ameponea kifo baada ya wakubwa wake wawili ambao wanadaiwa kuwa na visasi kutumia sehemu ya chini ya bunduki na kumpiga nayo kwenye kichwa mgongo na miguu na kumwacha akiwa hoi.
Akiongea katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi baada ya kukimbizwa huko na wasamaria wema, Ndirangu amesema kuwa wakubwa wake wameita polisi baada ya kumfanyia kitendo hicho kisha kuamurisha gari ya polisi kupita juu ya mwili wake baada ya kukaidi amri ya kupanda gari hilo.
Akithibitisha kisa hicho kamanda mkuu wa magereza kanda ya Pwani James Ngaira amesema kuwa afisa huyo amejeruhiwa baada ya utata kuibuka baina yake na wakubwa wake huku akiongeza kuwa uchunguzi tayari umeanzishwa kufuatia kisa hicho.
Taarifa na Radio Kaya.