Story by Ephie Harusi-
Afisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai nchini DCI, George Mitikowea Nangoye amefikishwa katika Mahakama ya Kilifi kwa madai ya kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 16.
Mahakama imeelezwa kwamba afisa huyo, alitekeleza kitendo hicho mnamo mwezi Septemba mwaka 2021 katika eneo la Marereni gatuzi dogo Magarini kaunti ya Kilifi.
Mahakama imebaini makosa manne katika kesi hiyo ambapo wa afisi huyo wa DCI anadaiwa kuyatekeleza ikiwemo kosa la unajisi, kutumia mamlaka yake vibaya, kunyanyasa kingono na kufanya uzembe.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Geoffrey Kimang’a, mshukiwa amekana shtaka hilo na Mahakama ikamuachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili ama pesa taslimu shilingi elfu 40.
Kesi hiyo itatajwa Januari 11 mwaka ujao.