Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.
Mombasa, Kenya , August 3 – Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 amefikishwa katika mahakama ya Mombasa akikabiliwa na kosa la kuiba bata.
Inaarifiwa kwamba kijana huyo kwa jina Omar Ali alimuiba bata huyo mwenye thamani ya shilingi elfu 1,500 mali ya Riziki Kadenge akiwa katika eneo la Jomvu kaunti ya Mombasa hapo jana tarehe 01 mwezi agosti mwaka huu.
Mshtakiwa amekiri shtaka hilo japo mamake mzazi akaiomba mahakama imsamehe akisema wanapitia hali ngumu kimaisha.
Hakimu mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Mombasa Richard Kagoni amemwachilia huru kijana huyo huku akimtaka mamake kumsajili katika taasisi za kiufundi ili ajipatie ujuzi.