Picha kwa hisani
Mbunge wa Garissa mjini Aden Duale amepokonywa wadhfa wa kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa na sasa nafasi yake imekabidhiwa mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya.
Mabadiliko hayo yamefanywa na Rais Uhuru Kenyatta alipoongoza mkutano wa wabunge wa jubilee katika jumba la KICC Nairobi,ambapo nafasi ya katibu wa muungano wa wajumbe jubilee iliokua ikishikiliwa na Kimunya sasa imekabidhiwa mbunge wa Eldas Aden Keynan.
Katika kikao hicho vile vile rais Kenyatta amesema siku ya alhamisi juma hili atatoa muelekea kuhusu nafasi za kamati za bunge la kitaifa zilizoachwa wazi baada ya walioshikilia nyadhfa hizo kutimuliwa.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa wadhfa huo wa kiongozi wa wengi bungeni, Kimunya ameshukuru rais Kenyatta kwa kumkabidhi wadhfa huo,huku akipongeza utendakazi wake mtangulizi wake Aden Duale akisema atatumia mbinu za duale kufanikisha majukumu yake.
Kwa upande wake Aden Keynan ambae ndie katibu mpya wa muungano wa wajumbe wa jubilee amepongeza mabadiliko hayo,akisema wanasiasa wote wanafaa kuzingatia sheria za vyama vyao.
Mkutano huo uliofanyika kwa chini ya dakika 30 umehudhuriwa na wabunge 179 ,naibu wa rais William Ruto pia ni miongini mwa waliohudhuria baada ya onyo kali kutoka kwa naibu mwenyekiti wa jubilee David Murathe dhidi ya kutohudhuria kutohudhuria.
Awali wabunge 126 kati ya 179 wa Chama cha Jubilee walitia saini ya kutaka Duale ang’atuliwe hasa kutokana na misimamo yake iliyoelekea kuzuia kufanikishwa kwa ajenda za Rais.