Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema ni lazima wakaazi wa kaunti hiyo wawe katika mstari wa mbele kukabiliana na itikadi kali ili kufanikisha jitihada za kuwazuia vijana wadogo kujiunga na uovu huo.
Achoki amesema vijana wengi wanajiunga na itikadi kali na ugaidi kutokana na tabia ya jamii na hasa wazazi kusalia kimya licha ya kuziona dalili hizo miongoni mwa watoto wao.
Akizungumza mjini Mombasa, Achoki amesema ni vyema iwapo jamii itafahamiana na kukumbatia ujirani mwema, hali itakayowawezesha kuwafichua wahalifu na magaidi miongoni mwao.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.