Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema kuwa oparesheni ya kiusalama itaimarisha katika kaunti hiyo ili kukabiliana na uhalifu unaotekelezwa na magenge ya kihalifu.
Kauli yake inajiri saa chache tu baada ya kundi la Wakali kwanza kuvamia wakaazi katika eneo la Bamburi ambapo watu wanane wamejeruhiwa kwa kukatwa kwa mapanga na kupigwa na vifaa butu.
Genge hilo limevamia maduka, nyumba za makaazi na watu waliyokuwa wakitoka kazini wakiwajeruhi na kuwaibia mali zao zikiwemo simu za rununu.