Kamishina wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewahimiza Wananchi kuwafichua vijana wanaotekeleza vitendo vya kihalifu katika sehemu za mashinani.
Akiongea mjini Mombasa Achoki amesema Visa vya uhalifu katika sehemu za mashinani vimeongezeka kufuatia ukosefu wa ushirikiano baina ya jamii na idara ya usalama.
Achoki amesema kuwa mkono wa sheria utawaandama vikali vijana watakaopatikana na hatia ya kutekeleza uhalifu.
Kamishna huyo w kaunti ya Mombasa amewahakikishia wakaazi usalama wa kutosha wanapoadhimisha siku kuu ya mashujaa.
Taarifa na Hussein Mdune.