Sekta ya uchukuzi wa umma mjini Malindi kaunti ya Kilifi imeathirika zaidi baada ya wasafiri kususia usafiri wa matatu kufuatia kupandishwa kwa nauli maradufu.
Wakiongea na wanahabari mjini Malindi baadhi ya wahudumu wa matatu wamesema kuwa hali hii imesambaratisha biashara zao.
Kwa upande wake Samuel Konde aliye mhudumu wa Matatu zinazohudumu kutoka Malindi hadi Mombasa ameiomba serikali kufutilia mbali ushuru huo kabisa badala ya kuupunguza kwa asilimia hamsini.
Nauli ya usafiri kutoka Malindi hadi Mombasa imepandishwa kutoka shilingi 350 hadi 450.
Taarifa na Charo Banda.