VANNELSARICK MADIBA BAYA , watu hawatakuelewa aidha labdha litakuwa ni jina la kigeni kwao, lakini unapotaja “ Ricky Melodies“ hapo watu wengi hasa washikadau na mashabiki wa muziki wa Bango watakuelewa kwa urahisi kuwa unamzungumzia msanii mkali sana anayefanya vizuri katika tasinia ya muziki wa Bango.
Ricky Melodies anafanya muziki wake wa bango katika studio za Ricky Records akiwa yeye mwenyewe ndiye prodiuza. Labdha usilolijua ni kuwa Ricky Melodies yuko na Band yake inayojulikana kama Fantansy Music. Katika safari yake ya uimbaji,yeye ndo Lead Singer wa band hii ya Fantansy Band.
Baada ya kuchezesha kikosi cha KDF nchini kwa wimbo wake wa KDF crew, alirudi studioni na kufanya wimbo uliovuma zaidi uliofahamika kama Bango Rifike,japo kuna baadhi ya mashabiki waliutohoa wimbo huu na kuupa jina jipwa la Bango Ridzulu kulingana na misitari fulani iliyotumika katika wimbo huu,wimbo huu uliopendekeza bango lifike hadi Somalia, kwa kweli ulikuwa ” Hit Song” kulingana na utani uliotumika kwenye misitari.
Safari hii aliamua kuungana na wasanii wengine wawili wanaofanya vizuri pia,wa kwanza akiwa ni ”Kaka Brayoo” aliyevuma na kibao chake ”Unanimala Maneno” wapili akiwa”Fadhil Bavyombo” anayejulikana kwa wimbo wake wa ”Kadzuchi” wote hawa waliungana na kufanya kolabo ya wimbo mpya unaoitwa ‘’Screen Short’’ wimbo huu ulipokamilika chini ya uongozi wa Ricky Melodies mashabiki waliupokea vyema kupitia RADIO KAYA ukichezwa kwa mara ya kwanza kabisa kwenye kipindi cha Misakato Ya Bngo chini ya nahodha DktrKeysherb a.k.a Dakitari wa Mapenzi.
Ricky – Melodies, The king of Nzele Music