Wakenya wanaotumia magari ya uchukuzi wa umma katika kaunti ya Kwale, sasa watalazimika kulipa nauli zaidi kutoka mjini Kwale hadi Mombasa.
Hii ni baada ya wahudumu wa magari hayo kuongeza nauli kutoka shilingi 130 hadi shilingi 200, kutokana na serikali kuwaagiza wahudumu hao kubeba abiria 8 pekee katika matatu za kubeba abiria 14.
Mmoja wa wahudmu wa magari hayo, Hamsisi Mwalimu Majaliwa amesmea wamechakua hatua hiyo ili kukidhi hali ngumu ya maisha.