Story by Ali Bakari –
Abiria mmoja ameaga dunia huku wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya gari waliyokuwa wameabiri kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Maji ya Chumvi kwenye barabara kuu ya Mombasa – Nairobi.
Afisa mkuu wa polisi eneo la Mariakani Ezekiel Chepkwony amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema ajali hiyo imehusisha basi ndogo na trela iliyokuwa kuwa ikitoka Mombasa kuelekea Nairobi na kugongana ana kwa ana.
Chepkwony amesema abiria wawili kati ya 12 waliojeruhiwa wamepata majeraha mabaya zaidi na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali tofauti katika eneo la Mariakani huku wengine wakipelekwa katika hospitali kuu ya rufaa kanda ya Pwani.
Hata hivyo polisi wamewahimiza madereva wa magari ya uchukuzi wa umma, kibinafsi na wale wa masafa marefu kuwa makini barabarani kwa kuzingatia sheria za trafiki ili kudhibiti ajali za mara kwa mara.