Abiria kadhaa wamejeruhiwa vibaya baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Spaki Kaunti ya Mombasa.
Kulingana na waliyoshuhudiwa ajali hiyo, matatu hiyo iliyokuwa ikitoka katikati mwa Mji wa Mombasa ikielekea Changamwe kabla ya kuepoteza mweleke na kugonga mlingoti wa stima na kubingiria mara kadhaa.
Dereva na Kondakta wake ni miongoni mwa waliyojeruhiwa katika ajali hiyo huku Onesmus Chonga dereva wa matatu iliyokuwa ikielekea Tudor akisema abiria wake wameponea.