Picha kwa hisani –
Abiria saba wametiwa nguvuni baada ya matatu waliyokuwa wameabiri kupatikana na vifurushi vya bangi katika eneo la Hindi Kaunti ya Lamu.
Naibu kamanda Mkuu wa polisi eneo la Hindi Sylvester Rotich amesema matatu hiyo kwa jina la ‘Baba Lao’ ilikuwa ikitoka Mombasa kuelekea Lamu.
Ni hapo polisi walipoikagua matatu hiyo na kupata vifurushi hivyo vya bangi, ambapo wamewatia nguvuni watu wote 7 waliokuwa ndani ya matatu hiyo, sawia na dereva wao.
Matatu hiyo inazuiliwa katika kituo cha polisi cha Hindi huku uchunguzi zaidi ukiidhinishwa kuhusiana na tukio hilo.