Jumla ya abiria 41 wamenusurika kifo jioni ya leo baada ya basi walimokuwa wakisafiria kushika moto.
Mkasa huo wa mwendo wa saa kumi na moja jioni umelihusisha basi la kampuni ya Tahmeed lililokuwa likitoka Jijini Nairobi likieakea Mjini Mombasa.
Kamanda mkuu wa trafiki katika Ukanda wa Pwani Emmanuel Okanda amesema kwamba abiria wote wametolewa salama bila majeraha yoyote kabla ya moto huo mkali kuliteketeza kabisa basi.
Kiini cha moto huo hakijabainika huku Okanda akisema kwamba visa hivyo vya mabasi kuteketea katika hali tata vimekithiri.
Tukio hilo linajiri Siku mbili tu baada ya basi moja la kampuni ya Dreamline kuteketea katika hali tata katika eneo la Macknon road katika Kaunti ya Kwale. Watu wawili wangali wanauguza majeraha mabaya ya moto katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani huku kiini cha mkasa huo kikisalia kitendawili.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.