Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wagombea wa ugavana katika kaunti ya Mombasa Ali Mbogo na Dkt William Kingi wamewakashfu wapinzani wao wa kisiasa huku wakisema hawastahili kumiliki uongozi wa kaunti hiyo.
Mbogo ambaye ni mbunge wa Kisauni na Kingi ambaye ni Naibu gavana wa kaunti hiyo ya Mombasa wamesema wapinzani wao Abdulswamad Sharif Nassir na Suleiman Shahbal hawana agenda yoyote ya kubadili maisha ya mkaazi wa kaunti ya Mombasa.
Kulingana na wanasiasa hao, mara nyingi mikutano ya kisiasa ya wapinzani wao imekumbwa na vurugu, hali isiyofaa kushuhudiwa katika kaunti ya Mombasa.
Mbunge huyo wa Kisauni amesisitiza umuhimu wa kampeni za amani katika kinyang’anyiro hicho cha Agosti 9 huku akionyesha matumaini ya kumrithi gavana wa sasa wa kaunti ya Mombsa Ali Hassan Joho.
Ikiwa hao kwasasa wavutana vutana ivo je mmoja wao akishinda ugovernor atakuwa na uongozo mzur kwel mombasa?upendo kwa wananchi waaza na viongoz wenyewe lakn shahbal na swamad wamefail wametuonesha n Tamaa ndo wako nayo.