Story by Gabriel MWaganjoni-
Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amewarai wabunge na Maseneta kutoka Pwani kushinikiza mashamba yanayoweza kutumiwa kwa kilimo cha unyunyizaji yakabidhiwe serikali za kaunti za Ukanda huu.
Nassir amesema usimamizi wa mashamba hayo utafanikisha kilimo cha kunyunyizia maji mashamba ili kulitosheleza eneo la Pwani kwa chakula.
Nassir amesema hali inayoukumba Ukanda wa Pwani kwa sasa ni ya kusikitisha kutokana na kiangazi cha muda mrefu, akisisitiza kwamba ni sharti kuwepo na mpangilio wa kilimo cha unyinyizaji maji mashamba kwa lengo la kuwakimu Wapwani kwa lishe.
Ameutaja mradi wa Galana/kulalu katika kaunti ya Tana River kama uliyostahili kumilikiwa na Serikali ya kaunti ili kutoa nafasi kwa Jumuiya ya kaunti za Pwani kupigania kilimo hicho kitakachozalisha chakula cha kutosha kwa Mpwani