Hisia mseto zimezidi kutolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa eneo la Pwani kuhusu na hatua ya Waziri wa Fedha nchini Henry Rotich ya kuongeza asilimia 16 ya ushuru wa mafuta nchini.
Wakiongozwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir, viongozi hao wameeleza kughadhabishwa na hatua hiyo, wakisema itawakandamiza wakenya walipa ushuru.
Akizungumza mjini Mombasa, Abdulswamad amedokeza kuwa hatua hiyo itachangia pakubwa kupanda kwa gharama ya maisha na akamtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati swala hilo na kutafuta suluhu.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.