Story by: Ngombo Jeff
Upanuzi wa hospitali ya Manuspaa ya Muyeye mjini Malindi kaunti ya Kilifi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hii ni baada ya Waziri wa afya wa kaunti hiyo Peter Mwarogo kufika mbele ya kamati ya utekelezaji ya bunge la kaunti hiyo na kueleza muda utakaotumika kukamilisha mradi huo.
Kulingana na Mwakilishi wa wadi ya Shella kaunti hiyo Twaher Abdulkarim, hatua hiyo inajiiri baada ya kupitishwa kwa mswada wa kuipanua hospitali hiyo miezi minne iliyopita.
Wakati uo huo Abdulkarim ameeleza kuwa mradi huo utafanyika katika awamu kadhaa na kukamilika ndani ya miaka miwili ijayo.