Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Tsimba/Golini katika kaunti ya Kwale Abdulaziz Burale amewataka vijana kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuidhinishwa rasmi na Tume ya IEBC, Abdulaziz amesema wakati ni sasa kwa vijana kuunga mkono vijana wenzio ambao wanagombea nyadhfa mbalimbali za uongozi ili kuchangia mabadiliko ya uongozi mashinani
Abdulaziz ambaye anawania kiti hicho kupitia tiketi ya chama cha UDA ameahidi kushirikiana na vijana katika kuwawezesha kibiashara na kujiimarisha kimaendeleo.
Hata hivyo amewahimiza wakaazi wa Tsimba/Golini na kaunti ya Kwale kwa ujumla kudumisha amani sawa na kujitenga na viongozi wenye nia ya kuwagawanya kwa misingi ya kikabila na dini.