Mtihani wa kidato cha nne (KCSE) ukiingia siku yake ya tano leo, watahiniwa pamoja wa wasimamizi wamezidi kuonywa dhidi ya kushiriki katika udanganyifu.
Akiongea na wanafunzi wa kitado cha nne katika shule ya upili ya Malindi kaunti ya Kilifi pamoja na watahiniwa 70 wa kibinafsi, Katibu mkuu msimamizi katika wizara ya mashauri ya kigeni Ababu Namwamba amehimiza watahiniwa kutoshawishika kudanganya kwenye mtihani huo.
Namwamba amewamotisha watahiniwa hao kutia bidii ili kuandikisha matokeo mema na kuregesha hadhi ya mitihani nchini baada ya kutiliwa shaka na wengi.
Amesema serikali imekabiliwa na kibarua kigumu kutafuta nyadhfa mbali mbali za kimataifa kwa wakenya wengi kutokana na kutiliwa shaka kwa hadhi ya mitihani ya Kenya.
Taarifa na Charo Banda.