Aliyekuwa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga amepinga vikali hatua ya zoezi la ukusanyaji sahihi za kulivunjilia mbali bunge la kaunti ya Mombasa chini ya vuguvugu la fagia bunge akisema kuwa linatekelezwa kisiasa.
Akiongea mjini Mombasa Gunga amehoji kwamba hiyo ni njama ya kuwatia hofu wawakilishi wa wadi ili washindwe kutekeleza majukumu yao ipaswavyo.
Aidha amesema kwamba huenda viongozi wanatumia hatua hiyo kutaka kufuja raslimali za umma kwani amesema kama kuna utata kwa mawaziri kuzembea kwenye majukumu yao ni jukumu la serikali kuwafikisha mbele ya kamati ya bunge hilo na kuchukuliwa hatua.
Akigusia swala la kufurushwa kazini zaidi ya wafanyikazi 400 kwenye idara ya mazingira kaunti ya kilifi gunga amesema kwamba hatua hiyo ilitekelezwa kinyume cha sheria na njia moja wapo ya kuwakandamiza haki zao.
Taarifa na Hussein Mdune.