Wakazi wa Kabelengani lokesheni ya Dagamra huko Magarini kaunti ya Kilifi wameamkia kilio baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 30 kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 27 na mwanawe umri wa miezi minne kabla ya kujitia kitanzi.
Babake marehemu Charo Kadenge amesema watatu hao walikuwa wamelala kwenye nyumba yake kabla ya kupatikana badaye ambapo Azan Charo kadenge amemchinja mkewe pamoja na mtoto kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujinyonga pia kwa kutumia nguo kwenye paa la nyumba yake.
Akithibitisha kisha hicho chifu wa eneo hilo Daniel Mrimi Kithi amesema marehemu aliyetekeleza unyama huo anashukiwa kuwa alikuwa akivuta bangi .
Aidha chifu huyo ameionya vijana na jamii kwa jumla dhidi ya kutumia dawa za kulevya huku akihimiza kutafuta ushauri kuhusu migogoro ya kinyumban.
Miili ya watatu hao imeondolewa na polisi na kupelekwa kwenye hifadhi ya maiti katika hospitali ya Malindi level 4 uchunguzi ukianzishwa.
Taarifa na Charo Banda.