Mwanakandarasi aliyejenga barabara inayotoka Changamwe kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa, ametakiwa kuharakisha ukarabati wa eneo la barabara hiyo lililoporomoka siku chache zilizopita.
Mwakilishi wa wadi ya Kipevu Faith Mwende Boniface amesema kwamba kuporomoka kwa barabara hiyo kumetatiza shughuli za uchukuzi hasa kwa magari yanayoelekea katika uwanja wa ndege.
Bi. Mwende anamtaka mwanakandarasi huyo awajibikie kazi yake.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.