Serikali ya kaunti ya Tana River itaekeza zaidi katika taasisi za kiufundi na vyuo vya kadri, ili kuhakikisha vijana wa kaunti hiyo wanapata ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amesema serikali yake inashirikiana na wadau mbalimbali wa kielimu nchini na kutoka mataifa ya kigeni, ili kuhakikisha hakuna vijana wanaosalia nyumbani.
Godhana amesema katika kipindi cha mwaka mmoja pekee, serikali yake imetumia kima cha shilingi milioni 6 katika kuboresha hali ya taasisi za kiufundi na vyuo vya kadri katika kaunti hiyo.
Aidha gavana Godhana amefichua kuwa idadi ya wanafunzi wanaojisajili katika vyuo hivyo kwa sasa imeongezeka kwa asilimia 45% na kufikia wanafunzi 458 ikilinganishwa na wanafunzi 307 mwaka wa 2016.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni