Picha kwa hisani –
Wazee wa Kaya za Mijikenda katika kaunti ya Kilifi, sasa wanasema Sherehe za kumuenzi Shujaa Mekatilili wa Menza za kila mwaka, huenda zikaandaliwa kwa njia tofauti ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Mwenyekiti wa Chama cha kitamaduni wa MADCA, Emmanuel Munyaya amesema sherehe hizo bado hazijaihirishwa japo watakaohudhuria ni watu wachache kinyume jinsi zinavyokuwa zikisheherekewa.
Akizungumza na Wanahabari kule Malindi, Munyaya amesema sherehe hizo zitaadhimishwa rasmi katika eneo la Shaka hola tarehe 13 mwezi huu mahali ambapo shujaa huyo alimpiga kofi mkoloni.