Picha Kwa Hisani –
Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya ameshikilia kuwa mswada tata wa ugavi wa raslimali za umma kwa serikali za kaunti unafaa kupata suluhu la haraka ili kufanikisha maendeleo mashinani.
Gavana Mvurya amesema ni wakati sasa kwa maseneta kuelewana kuhusiana na mvutano wa mswada huo tata kwani kaunti nyingi zimeshindwa kuwatekelezea wananchi maendeleo.
Wakati huo uo amependekeza serikali za kaunti za Pwani kuendelea kupata mgao wa juu wa raslimali kutoka kwa serikali kwani tayari bajeti ya za serikali za kaunti hizo zimetengezwa.