Askofu Lagho: Sio vizuri kuchoma nyumba za ibada
Askofu wa Kanisa katoliki jimbo la Malindi Willybard Lagho amelaani vikali kitendo cha uvamizi na kuteketezwa kwa kanisa la PCEA na msikiti wa Alaska katika eneo la Kibra jijini Nairobi siku ya Jumatatu.
Askofu Lagho ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo hicho huku akikitaja kama kitendo cha uharibifu wa maeneo ya kuabudu.
Lagho aidha amedokeza kwamba huenda kitendo hicho kimetokana na mzozo uliopo kuhusu umiliki halali wa maeneo ya Kanisa na Msikiti huo.
Wakati uo huo ametoa wito kwa waumini wa dini ya kikristo na ya kiislam humu nchini kushirikiana na viongozi katika kutafuta suluhu la mzozo huo.