Muigizaji maarufu wa vihoja Mahakamani ameaga dunia.
Story by Our Correspondents-
Muigizaji maarufu na mkongwe humu nchini Gibson Gathu Mbugua ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 56.
Mbugua alifahamuka sana kama Kiongozi wa mashtaka {Prosecutor} katika kipindi cha Vioja Mahakamani kinachopeperushwa katika runinga ya kitaifa ya KBC ameaga dunia baada ya kuugua kwa miaka 20 ugonjwa wa kisukari na matatizo ya figo.
Mbugua ambaye alifanyiwa upasuaji na kubadilishiwa figo alikuwa anaendelea vizuri hadi kifo chake ambacho kimeshtusha wengi na kuchangia pengo kubwa katika Sanaa ya uigizaji.
Familia ya mbugua imethibitisha kifo chake na kusema kwamba mwendazake amefariki dunia mapema leo.
Hata hivyo wakenya wa tabaka mbalimbali wamejitokeza na kutuma rasala zao za rambirambi kwa familia ya Mbugua.