Dogo Richie: Nataka kufunga ndoa na Azziad
Dogo Richie amefichua kwamba ana hisia za mapenzi kwa mwanamitandao Azziad Nasenya na kueleza kwamba angependa kufunga ndoa naye.
Mkali huyo wa muziki anayetamba kwa ngoma yake mpya #TuleSheshe amefichua kwamba alimpenda mara ya kwanza alipomuona Azziad kupitia mtandao wa TikTok kupitia mahojiano ya moja kwa moja kwenye kituo kimoja cha habari jijini Nairobi.
Mwanamuziki huyo pia alifunguka kwamba mara kwa mara amekuwa akimuota mwadada huyo aliyejizolea umaarufu mitandaoni kupitia #UtawezanaChallenge kwenye TikTok
Aidha Richie alimuomba Azziad kulifanyia kazi ombi lake ikiwa hayupo kwenye mahusiano ya kuelekea kwa ndoa na kuahidi kutomchezea.
Pia soma: https://radiokaya.co.ke/dogo-richie-kwenye-bifu-kali-na-ringtone/