Watu milioni 8 uaga dunia kila mwaka kutokana na utumizi wa tumbaku
Story by Mimuh Mohammed –
Shirika la Afya duniani WHO limeeleza kwamba watu milioni 8 hufariki kila mwaka ulimwenguni kutokana na utumizi wa bidhaa zinazotokana na tumbaku.
WHO katika ujumbe wake wakati maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi tumbaku duniani, limebainisha kwamba Tumbaku pia limechangia uharibifu wa mazingira na afya ya binadamu kupitia ukuzaji, usajilisha, usambazaji na utumizi wa bidhaa za tumbaku.
Katika ripoti hiyo inayoangazia athari ya Tumbaki WHO vile vile imesema kufikia sasa miti milioni 600 imekatwa kwa ajili ya kutengeneza tumbaku huku tani milioni 84 za hewa kaa inayotokana na moshi wa sigara ikichangia kupanda kwa joto duniani.
Wizara ya afya nchini imeandaa hafla ya kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani katika chuo kikuu cha Nairobi, ambapo mkurugenzi wa afya nchini Dkt Patrick Amoth ni kati ya wanaohudhuria hafla hiyo na kusisitiza haja ya wakenya kujitenga na matumizi ya tumbaku.