Kampuni ya Coca cola kuwajenga uwezo zaidi ya wanawake na vijana, Jomvu
Story by Ali Chete-
Jumla ya Wanawake na vijana 2500 katika gatuzi dogo la Jomvu kaunti ya Mombasa wanatarajiwa kunufaika na mafunzo tofauti ya kibiashara ili kujikimu kimaisha.
Afisa wa kiufundi wa kampuni ya Coca-Cola Jane Gishanga amesema mradi huo unalenga vitongoji duni katika kaunti hiyo na vijana na wanawake watawezeshwa kujikimu kimaisha kupitia mradi huo ambao utagharibu shilingi milioni 28.
Afisa huyo amedokeza kwamba ushirikiano na Shirika la Shinning For Communities yaani SHOFCO utawezesha kuwapa mafunzo wanawake na vijana ili kuanzisha miradi itakayowajenga uwezo.
Kauli yake imeungwa mkono na Afisa wa Miradi katika Shirika la SHOFCO Gladys Mwendee aliyesema watawasaidia walengwa hao kujiunga katika makundi ya kibiashara.