
Mahakama ya Shanzu imemhukumu kifungo cha maisha mshukiwa wa dawa za kulevya
Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mahakama ya Shanzu imemhukumu mwanamke mmoja mashukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya kifungo cha maisha gerezani na pia kumuamuru alipe faini ya shilingi milioni 22.1.
Hakimu mkaazi wa mahakama ya Shanzu David Odhiambo amesema Fatuma Sicobo Mohammed alinaswa na kilo 2.4 za dawa za kulevya aina ya Heroine katika eneo la Shanzu mwaka wa 2019.
Odhiambo amesema ushahidi uliyotolewa mahakamani umethibitisha kwamba Fatuma alikuwa na dawa hizo za kulevya nyumbani kwake na akazitupa kupitia dirishani pindi alipowaona maafisa wa kitengo cha kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Hata hivyo, Mahakama amemuachilia huru mshukiwa wengine Masuo Bakari Tajiri kufuatia kukosekana kwa ushahidi wa kumhusisha na kesi hiyo.
Mahakama imetaka dawa hizo za kulenya kuharibiwa kabla ya tarehe 30 mwezi Januari mwaka wa 2022, huku ikitaka faini hiyo ya shilingi milioni 22.1 ilipwe kabla ya Fatuma kuanza kutumikia kifungo chake cha maisha gerezani.