Kenya imepokea chanjo ya Corona aina ya Pfizer kutoka Marekeni
Story by Our Correspondents –
Kenya imepokea shehena nyingine ya chanjo ya Corona aina ya Pfizer yenye dosi 990,990 kutoka taifa la Marekeni ili kupiga jeki juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea shehena hiyo ya Chanjo ya Corona katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Katibu mkuu msimamizi katika Wizara ya Afya nchini Dkt Mercy Mwangangi amesema chanjo hiyo itasambazwa katika kaunti zote nchini.
Dkt Mwangangi amesema kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu, Kenya itakuwa imepokea dozi milioni 5 ya chanjo ya Corona aina ya Moderna, Pfizer na Johnson na Johnson kutoka taifa la Marekani.
Wakati uo huo amesema kufikia siku ya Alhamis wakenya 5,226,128 tayari wamepokea chanjo ya Corona huku akiwahimiza wakenya kutopuuza chanjo hiyo na badala yake kujitokeza na kupokea chanjo.