
Familia mbili kaunti ya Mombasa zalilia haki
Story by Ali Chete –
Familia mbili kutoka kaunti ya Mombasa zinalilia haki baada ya jamaa wao kupotea katika hali tatanishi takriban miezi miwili na kujulikana waliko.
Familia ya Abshir Garo Ali na Jackson Njue zimesema wawili hao walitoweka mnamo tarehe 24 mwezi Julai hadi sasa hawajulikani waliko licha ya juhudi za familia hizo kuwatafuta.
Kulingana na Dhahabu Hasasan ambaye ni mamake Abshir Garo, watu waliojitambulisha kama maafisa wa polisi walimchukua wanawe na kumpiga mbele yake huku wakidai kwamba wanampeleka katika kituo cha polisi Central jijini Nairobi.
Kwa upande wake Charles Njue ambaye ni kakaye Jackson Njue aliyetekwa nyara katika eneo la Diani kaunti ya Kwale tarehe sawa na ile yaliotekwa Abshir amesema kakake hajawahi kujihusisha maswala ya uhalifu.
Akizungumzia swala hilo Naibu mkurugenzi wa Shirika la Haki Africa Salma Hemed amesema visa vya watu kupotezwa katika hali tatanishi vimekithiri mno, huku akidai kuwa kati ya mwezi Januari hadi sasa wamenakili visa 34.