Matiang’i ameagizwa kufika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu usalama kuhojiwa
Story by our Correspondents –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi nchini Hillary Mutyambai wameagiza kufika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu usalama siku ya Jumatano kujibu maswali kuhusu usalama wa taifa.
Kamati hiyo inayoongozwa na Peter Mwathi ambaye pia ni Mbunge wa Limuru inataka ufafanuzi zaidi kuhusu mikakati iliyoweka ya kiusalama nchini.
Kamati hiyo inataka pia kuelezwa hatua zilizochukuliwa za kubadilisha maafisa wa usalama waliokuwa wakilinda makaazi na Naibu Rais Dkt William Ruto.
Kulingana na barua iliyoandikwa na Karasi wa bunge la kitaifa Michael Sialai, kubadilishwa na walinzi waliokuwa walinda makaazi na Naibu rais ni swala lenye uzito na linahitaji kujadiliwa.