KNUT kupinga kurejeshwa kwa viboko
Picha kwa hisani –
Chama cha walimu wa shule za msingi nchini KNUT kimesema kitapinga mpango wa kurudishwa kwa adhabu shuleni wakati huu ambapo kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya ukosefu wa nidhamu.
Kulingana na katibu mkuu wa chama hicho nchini Wilson Sosion ni kuwa kauli ya waziri wa elimu nchini prof George Magoha kutaka kurudisha fimbo darasani ni suala lililopitwa na wakati.
Akizungumza katika uwanja wa michezo wa Afraha jijini Nairobi wakati wa uchaguzi wa chama hicho Sossion amesema walimu hawatakubali kuwaadhibu wanafunzi kwani adhabu italeta uhasama kati ya pande hizo mbili.
Wakati uo huo Sossion amewalaumu wazazi kwa kuchangia ongezeko la visa vya ukosefu wa nidhamu kwa watoto huku akisema kuwa walikosa kuwaelekeza wakati walipokuwa nyumbani kipindi cha miezi kumi ya janga la Corona.