
Wizara ya Afya kaunti ya Kwale yaihimiza jamii kutembelea vituo vya afya
Picha kwa Hisani –
Wizara ya Afya kaunti ya Kwale imeihimiza jamii ya kaunti hiyo kutembelea vituo vya Afya kupata huduma mbalimbali za kimatibabu na wala sio kuhufikia mlipuko wa janga la Corona.
Afisa wa Afya anayesimamia masuala ya afya ya uzazi katika gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale Dima Galole amesema takwimu kutoka Wizara hiyo zimeonyesha kuwa mwezi Machi hadi Juni huduma za matibabu zilikuwa zimeshuka.
Wakati uo huo afisa huyo wa afya amesema wizara hiyo imeeka mikakati mwafaka ya kuhakikisha wagonjwa wanaotembelea vituo vya afya wanatii masharti ya kudhibiti Corona.