
Viongozi wa kidini wakutana na wadau wa afya kujadili mbinu za kuzuia corona
Picha kwa Hisani
Viongozi wa kidini, Maafisa wa idara ya Afya na wale wa kiusalama wamefanya mkutano wa kutathmini jinsi ya kuzuia maambukizi ya Corona kwenye nyumba za ibada katika eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa.
Wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la ‘Jesus Winning Ministry’ Daniel Indatula, viongozi hao wamesema makanisa yamezingatia kikamilifu masharti yaliowekwa na Wizara ya Afya.
Kwa upande wake Chifu wa eneo la Chaani Ben Valasa Mutunga amesema baadhi ya masharti hayajazingatiwa katika nyumba za ibada lakini mazungumzo hayo yatoa muelekeo juu ya suala hilo.
Mkutano huu umejiri baada ya taarifa za kukanganya kuenea kuwa kuna baadhi ya makanisa yamekuwa yakikiuka masharti yaliowekwa na Wizara ya Afya nchini ya kudhibiti maambukizi ya Corona.